Hali ya msongamano inazidi kushugudiwa katika kivuko cha likoni ferry asubui ya Leo ya tarehe 28 mwezi wa pili mwaka wa elfu mbili ishirini na nne baada ya trela lililokuwa likivuka kuelekea Tanzania kutoka Mombasa kushindwa kuukwea mlima huo.

Licha ya ferry nne leo kuwa kwenye zamu ya kuvusha egesho hilo ambalo ferry ya MV kwale imesalia ndio imesababisha ferry zengine MV Harambee MV Jambo na MV safari kukosa egesho Kwa wakati.Visa kama hivi sio mara ya Kwanza kushughudiwa katika kivuko cha ferry majuma kadhaa hali sawia na hio pia ilitokea .

Je shirika la huduma za ferry ambalo sasa lipo chini ya bandari ya Mombasa limechukua hatua gani kukabiliana na hali kama hizo? Miaka nenda miaka rudi Kenya ferry haijaweka gari la dharura almaaruf “breakdown”ambapo lingesaidia pakubwa kuyavuta magari yanayokwama.

Matumaini sasa yamesalia Kwa barabara ya dongo kundu ambayo inasemekana hivi karibuni itakuwa inafunguliwa rasmi baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.Barabara hio itapunguza pakubwa msongamano wa magari kwani barabara hio itaunganisha bonje na ukunda kwa urahisi.


Wakazi wengi wa Mombasa na viunga vyake walitarajia daraja lilijengwa likiunganisha likoni lingetatua changamoto zao lakini halikudumu.Awali hali ya msongamani ilikuwa imepungua kwani wengi walikuwa wakivuka kutumia daraja hilo la kuelea liwatoni floating bridge lakini sasa kila mmoja ametegemea kivuko cha ferry.

Mwaandishi: Edwin Mwandau

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *